Na Imelda Mtema
Msanii wa kitambo katika anga la sanaa hapa Bongo, Nasra Mohammed ‘Dina’ ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa, akibeba mimba wakati akijifungua atajirekodi ili dunia nzima ione inavyokuwa.
Dina aliliambia Ijumaa kuwa yeye na mchumba wake wameamua kufanya jambo hilo ili watu wengine wajifunze umuhimu wa kuwaheshimu wake zao.
“Mimi na mpenzi wangu tumekubaliana hilo kwa sababu miezi miwili ijayo nimepanga kushika ujauzito Mungu akinibariki, siku ya kujifungua nataka ulimwengu uone, najua itakuwa fundisho kwa wengine,” alisema Dina.
