James DeBarge
Aliyekuwa mume wa zamani wa Janet Jackson, James DeBarge ameibuka na kudai kuwa aliwahi kumpa mimba Janet lakini mwanadada huyo akambambikia mtu mwingine.
Maneno hayo yamekuja baada ya Janet kutangaza kuwa ni mjamzito wa mtoto wa kwanza kwa mumewe mpya aitwaye Wissam Al Mana
.
Janet Jackson na James DeBarge
Kufuatia taarifa hiyo, James aliuambia Mtandao wa Radar Online kuwa, aliwahi kuzaa na Janet lakini baada ya mtoto huyo kupewa mwanaume mwingine, alipokuwa mkubwa hivi karibuni alimpigia simu na kumwambia yeye ndiye baba yake.
“Kwa Janet huyo si mtoto wa kwanza kwa sababu kuna mtoto mwingine ambaye nilizaa naye, akamgawa kwa mtu mwingine na mpaka sasa Janet hapendi kuniambia kwa sababu ya woga,” alisema James.
