×

Mchepuko atajwa kuivunja ndoa ya Steve RnB

482199_528821560503557_253025517_nSteve RnB

Stori: Imelda Mtema
Kumekuwa na madai kuwa ndoa ya Mwanamuziki Steve RnB na mkewe Esther imevunjika huku demu mmoja aliyetajwa kwa jina la Neema Shadrack akidaiwa ndiyo chanzo.

Safu hii iliwatafuta wote kuzungumzia sakala hilo, wasikie hapa chini:
Steve: “Hakuna mtu ambaye aliingia katikati na kuharibu ndoa yetu ni ugomvi uliokuwepo baina yetu na sasa tupo katika harakati za kupeana talaka maana hatuishi wote zaidi ya miezi nane.”
Esther (mke)

“Mimi namjua huyo msichana kwa kumsikia na kumuona kwenye mitandao ya kijamii na kweli ndoa yangu ipo kwenye mgogoro ila namuachia Mungu.”
Neema (Mchepuko)

“Ndoa ya Steve ilikuwa kwenye mgogoro hata kabla mimi sijakuwa na uhusiano naye hivyo mimi siwezi kuwa chanzo cha ndoa yao kutibuka.”

Leave a Comment