Jide.
HAMIDA HASSAN
Kuna wakati f’lani niliwahi kuandika makala ambayo ilikuwa inawahusu wasanii wa kiume Bongo ambao walitunga nyimbo na kuamua kuchanana ukweli ikiwa ni njia ya kuwashika mashabiki wao. Walifanya hivyo ‘Diamond’ na ‘Nay wa Mitego’ kwenye wimbo wao wa Muziki Gani. Wakagonga kolabo yao nyingine ya wimbo wa Mapenzi au Pesa.

Aliyekuwa mume wa Jide, Gardner.
Ukiacha hao, Jux na Ben Pol nao juzikati wakaibuka na ngoma yao iitwayo Nakuchana. Ndani ya nyimbo hizo wasanii hao wameambiana ukweli, wakafikia hatua ya kuumbuana kwenye mambo ambayo inawezekana isingekuwa muziki wangerushiana ngumi.
Shilole na Nuh Mziwanda
Nikagundua kuwa, kupitia nyimbo hizo wasanii hao wanajiongezea mashabiki kwa kuwa watu wengi wanapenda kusikiliza na wakati mwingine wananunua kutokana na kuvutiwa na mashairi. Ndiyo maana umeona jinsi ngoma hizo zilivyokiki ndani ya muda mfupi baada ya kutolewa.
Lakini kwa wasanii wa kike nao wamekuja na kastaili kao f’lani ka kuwachana wapenzi wao baada ya kuachana kupitia nyimbo. Kuna kitu kinaitwa vijembe ambapo mara kadhaa tumezoea baada ya wapenzi kuachana unaweza kukuta mmoja anatoa maneno ambayo yanaashiria wazi ni vijembe kwa mpenzi wake.
Linah.
Sasa hivi imekuwa ni tofauti kidogo, baadhi ya mastaa wameanzisha staili ya kutunga nyimbo ambazo ukifuatilia kwa makini mashairi yaliyomo utagundua ni vijembe kwa wapenzi wao waliowaacha. Miaka ya nyuma sana aliwahi kufanya hivyo Nature pale alipomuimba mpenzi wake Sinta kwenye wimbo uitwao ‘Inaniuma sana’, ikawa kimya kidogo.
Mara tukamsikia Linah naye akimuimba Amini kwenye ule wimbo wake wa Bora Nikimbie. Hivi karibuni gumzo kubwa ni kuhusu wimbo wa Jide wa Ndi Ndi Ndi ambapo ukisikiliza mashairi na ukiangalia kideo chake utathibitisha kuwa ni dongo la wazi kwa aliyekuwa mumewe, Gardner.
Shilole naye
Alipoachana na Nuh akawa kimya kidogo lakini kumbe alikuwa akifikiria amchane vipi zilipendwa wake huyo. Mara juzikati akaibuka na wimbo mpya uitwao Say My Name. Ndani ya wimbo huo Nuh amekula za chembe za kutosha.
NI SAHIHI?
Watu wengi wamekuwa na kasumba ya kuwasema vibaya wapenzi wao baada ya kuachana lakini wengi wamekuwa wakitoa maoni yao na kusema siyo sawa! Kuanika udhaifu wa mpenzi wako hakuna faida yoyote kwa kuwa, hata kama utamuaibisha, wewe pia utaaibika kwa kuonekana limbukeni.
Nasema huo usiwe utaratibu hasa kwa mastaa kutungiana nyimbo na kusemana vibaya baada ya kuachana. Ikiwa hivyo mtawafanya wanaume wawaogope na hata wale akina Nahreel ( mpenzi wa Aika), Jux (mpenzi wa Vanessa) wawe na hofu wakijua kuwa wakimwagana watachanwa.




