Mshindi wa Shindano la Shika Ndinga na Efm, Espedito Jackson (kulia) akikabidhiwa ufunguo na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda baada ya kuibuka kidedea.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akimshuhudia mmoja wa washindi wa Shika Ndinga aliyejishindia Gari aina ya Suzuki Carry, Rose Antony.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Makonda akiwapongeza washindi waliopatikana katika hatua za mashindano yaliyofanyika katika wilaya tano, Kinondoni, Kibaha,Bagamoyo,Temeke na Ilala.
Wakiendelea kupongezwa.
Washiriki wa Shindano la Shika Ndinga wakiwa katika mashindano.
Washiriki wakiendelea na mashindano ili kumpata mshindi wa Shika Ndinga.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Efm Radio wakifuatilia mashindano hayo.
Shindano la Shika ndinga lililokuwa likiratibiwa na kituo cha Redio Cha Efm kilichopo Kawe jijini Daers Salaam, jana Jumamosi lilifikia tamati baada ya washindi walioibuka kidedea kuchukua Ndinga aina ya Suzuki Carry ambao ni, Espedito Jackon na Rose Antony wote wakitokea Wilaya ya Kibaha-Pwani.
Shindano hilo lilifikia tamati jana katika Viwanja vya TP Sinza jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza kwenye hafla hiyo , Meneja Mkuu wa Efm redio, Dennis Ssebo alisema kuwa washiriki 10 kutoka kila wilaya kati yao wanawake watano na wanaume watono ambao walipatikana baada ya mashindano yaliyofanyika kwenye wilaya zao waliingia katika fainali kushindania gari aina ya Suzuki Carry.
Washindi hao, Espedito Jackon na Rose Antony walipatikana katika raundi ya pili ya kushika glasi ya maji mkono mmoja na mguu mmoja ukiwa umekunjwa huku mkono nao ukishikilia ndinga wakati katika raundi ya kwanza washiriki walishika chupa za maji hadi anayeshindwa kuvumilia anakuwa amejitoa katika mashindano hayo.
Akikabidhi zawadi kwa washindi waliopatikana katika shindano hilo, Mgeni rasmi ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alisema kuwa anawapongeza kituo cha redio cha Efm kwa kuanzisha mashindano ambayo yanawanufaisha wananchi kutoka hatua moja na kwenda nyingine hivyo akisema wanapaswa kuigwa na watu wengine.
“Ninyi washindi wa zawadi za magari hayo na pikipiki nawaombeni mkayatumie katika kuongeza vipato vyenu ili familia zenu ziweze kunufaika na zawadi hizo na si kwa kufanyia mambo yasiyo kuwa ya msingi,” alisma Makonda.
Kwa upande mwingine Meneja wa Efm Dennis Ssebo aliongeza kuwa lengo la shindano hilo lilikuwa ni kuwawezesha wasikilizaji wa Efm kwa namna moja au nyingine kuongeza na kukuza vipato vyao katika kuchangia kuimarisha maisha yao kupitia zawadi walizoibuka nazo.
(Na Denis Mtima/Gpl)









