KATIKA kile kinachoonekana ni utani wa kuongezeka kwa magari katika barabara nchini China, dereva mmoja amepigwa faini kwa kuendesha lori moja ambalo lilikuwa limebeba magari mengine mawili juu yake.
Kwa mujibu wa kituo cha serikali cha televisheni za CCTV, polisi wa doria katika barabara moja kuu katika Jimbo la Shanxi kaskazini mwa China, walimpiga faini dereva huyo kwa lori lake kuzidisha mzigo kinyume na sheria na hivyo kuhatarisha usalama barabarani.
Televisheni hiyo ilieleza kwamba, dereva huyo aliyekuwa amefanya hivyo ili kukwepa gharama kubwa za kusafirisha magari matatu alipigwa faini ya Dola 30 (yuan 200) kwa kitendo hicho na akapigwa faini nyingine kutokana na kasoro katika leseni yake ya udereva.

Baada ya picha hiyo kuwekwa katika mtandao, watu walitoa maoni yao ambapo wengine walisema adhabu ilikuwa ni ndogo mno na wengine walisifia kitendo hicho kama ni ubunifu wa kusafirisha magari makubwa.
Mwezi Novemba mwaka jana, malori mawili madogo yalikutwa yakiwa yamebeba malori madogo mawili juu yake katika barabara moja kuu katika jimbo la Anhui ambapo madereva husika walipigwa faini kwa kukiuka uzito wenye kubebwa na magari hayo na kukiua urefu wa kwenda juu unaotakiwa katika magari yenye kupita barabara hiyo.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz
