The House of Favourite Newspapers

Shetta, Ali Kiba waingia vitani

0

Ali-Kibaaaaaaaaaa-333

Ali Kiba

Hans Mloli, Dar ess Salaam

SAFARI hii siyo Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ali Kiba bali imekuwa ni Ali Kiba dhidi ya Shetta waliojikuta wakiingia kwenye vita kubwa ya ushindani iliyotokana na video zao zilizotoka hivi karibuni. Kiba ameachia video ya Aje na Shetta ametoa ya Namjua.

Video za wasanii hao ambazo zote zimefanyika nchini Afrika Kusini ziliachiwa rasmi wiki iliyopita lakini ile ya Aje inapigwa kwenye runinga ya MTV na kwenye TV za Kibongo itaanza kuonyeshwa kesho Alhamisi,  tayari zimezua gumzo kubwa sehemu mbalimbali hasa kwenye mitandao ya kijamii.

shetta

Shetta

Ukiachana na ubora wa video hizo zilizoonekana kuwabeba wote wawili lakini wengine walimsifia Shetta katika uchezaji na hata mpangilio wa video yake, waliokuwa upande wa Kiba nao walipongeza uvaaji wake na maudhui ya maisha ya kifahari yaliyoendana na ujumbe wa wimbo huo.

“King Kiba umefanya balaa sana katika hii video, nafikiri huu ni mwanzo wa safari iliyokuwa ikihitajika kwa muda mrefu,” aliandika mmoja wa watumiaji wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram kwenye akaunti ya Kiba iliyokuwa na moja ya ‘post’ zinazotambulisha wimbo huo.

Lakini dakika chache baadaye akaibuka mwingine katika post hiyo na ku-comment: “Itakuwa hamjaiona Namjua ya Shetta ndiyo maana mnaisifia Aje.” Hali hiyo iliamsha hisia za wengi na kuzaa malumbano makubwa kila mmoja akisema lake kuhusiana na video hizo.

Leave A Reply