The House of Favourite Newspapers

Wakongwe wa Muziki ‘Waikalisha’ Dar Live

0

Wakongwe wa Muziki (1)

Abby Skills akiwakumbushia mashabiki wimbo wa Maria.

Wakongwe wa Muziki (2)

Dully Sykes akiwapagawisha mashabiki.

Wakongwe wa Muziki (3)

Juma Nature akigonga ‘nyundo’ zake.

Wakongwe wa Muziki (4)

Mabaga Fresh nao wakiwakumbusha mashabiki ‘wakati huo’.

Wakongwe wa Muziki (5)

Soggy akiimba na kuserebuka.

Wakongwe wa Muziki (6)

 Shabiki akiwa amevamia jukwaa kumtunza Dully.

Wakongwe wa Muziki (7)

Soggy akiendeleza libeneke.

Wakongwe wa Muziki (8)

    Juma Nature akikamua na Inspekta Haruni.

Wakongwe wa Muziki (9)

 Inspekta akiendeleza burudani.

Wakongwe wa Muziki (10)

Suma G akionyesha kipaji chake cha kuimba.

ONYESHO la wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao waliwahi kutamba enzi zao, usiku wa kuamkia leo walitoa burudani kali katika Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam, ambapo mashabiki walionjeshwa tena utamu ulioanzisha muziki wa vijana nchini.
Moto wa furaha uliwaka katika onyesho hilo baada ya mashabiki kukumbushiwa enzi ambazo muziki huo uliibuka hapa Bongo.  Baadhi ya wanamuziki ambao walitoa burudani ni Abby Skills, Juma Nature, Dully Sykes, Soggy Dog, Mabaga Fresh, Manzese Crew, Suma G, Zin Zag Crew, Solid Ground Family na Rama Mluguru.

(NA ISSA MNALLY)  

Leave A Reply