Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa SG Entertainment, Victor Mkumbo (kushoto) akizungumza kwa waandishi wa Habari (Hawapo pichani) wakati wa utambulisho huo wa Miss Chang’ombe 2016. Kulia ni Mratibu wa shindano hilo, Bwana Adam Hussein .
Mratibu wa shindano hilo la Miss Chang’ombe, Bwana Adam Hussein (kulia) akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) juu ya shindano hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa SG Entertainment, Bwana. Victor Mkumbo
Mratibu wa shindano hilo la Miss Chang’ombe, Bwana Adam Hussein (Katikati) akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) juu ya shindano hilo. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa SG Entertainment, Bwana. Victor Mkumbo na Kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo ya SG, Bwana. Geofrey Mbalazi
… warembo katika mapozi na mahojiano.
Mchakato wa kumsaka mrembo wa Kitongoji cha Changombe (Miss Chang’ombe) 2016 unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Juni 2, 2016 ambapo warembo wenye sifa na vigezo, wataanza kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania taji hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Ukumbi wa New Habari Maelezo, Posta jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Kampuni ya SG, waandaaji wa shindano hilo, Victor Mkumbo alisema fomu zinapatikana kwenye Duka la Nguo la Chilu Latest Wear, Temeke Mwisho, CDS Park (zamani TCC Club Chang’ombe) na Mpo Afrika, Davis Corner jijini Dar es Salaam.
“Warembo watano kutoka Chang’ombe wataungana na warembo kutoka vitongoji vingine viwili vya Kigamboni na Mbagala kuwatafuta warembo wa Temeke na baadaye mrembo wa Tanzania kwa mwaka huu.
“Nawasihi warembo wanaojiona wanazo sifa na vigezo, wenye umri wa kuanzia miaka 18 hadi 24 wajitokeze kwa wingi kuchukua fomu kwenye vituo tulivyovitaja hapo juu kwa ajili ya kushiriki, na washindi watano wa mwanzo watapata nafasi pia ya kulipiwa karo ya chuo,” alisema Mkumbo.
Na Mwandishi Wetu/ GPL



