The House of Favourite Newspapers

Aliyetumbuliwa na JPM anunua benzi la mil.75

0

rungweWakili Hashim Rungwe.

DAR ES SALAAM: Kigogo mmoja wa bandari aliyetumbuliwa na Rais Dk. John Magufuli ‘JPM’ hivi karibuni amejinunulia gari la kifahari aina ya Benz lenye thamani ya shilingi milioni 75.

Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake hivi karibuni katika mahojiano maalum, Mwenyekiti wa Taifa wa Umma Party ambaye pia ni mfanyabiashara wa kuuza magari, Wakili Hashim Rungwe alisema kigogo huyo alinunua Benz hilo kwa ajili ya matumizi yake binafsi licha ya kudhaniwa kuwa, kwa sasa angekuwa hana kitu.

“Kiujumla utumbuaji wa majipu sioni faida yake kwa wananchi wa kawaida kwa sababu wote waliotumbuliwa wanapata mishahara yao kama kawaida na hivi karibuni kigogo mmoja wa bandari alikuja kwangu kwenye yadi na kununua Benz la thamani ya shilingi milioni 75,” alisema Wakili Rungwe bila kumtaja jina kigogo huyo.

Aliongeza kuwa, utumbuaji majipu bado haujasaidia kuondoa njaa kwa wananchi wa kawaida badala yake ameshuhudia waliotumbuliwa wakiendelea ‘kutanua’ mitaani na kula mishahara yao bila kuifanyia kazi.

Alisema kuwa, wakati wa kufanya manunuzi ya gari hilo, kigogo huyo  alimwambia kuwa, kwa sasa kila akiamka anafikiria kwenda kutumbua maisha wapi.

“Alisema yeye na familia yake ni bata tu siku hizi, maana wakati mwingine anakwenda ufukweni na mkewe na watoto wote. Kifupi aliniambia hajapata athari zozote kwa kutumbuliwa,” alisema Rungwe kwa mshangao mkubwa.

Hivi karibuni serikali imewatumbua vigogo wengi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania na wale kutoka Kodi ya Mapatao TRA kwa kuwasimamisha kazi kwa madai kwamba waliwasaidia wafanyabiashara kukwepa kulipa kodi hivyo kuikosesha serikali mabilioni ya shilingi.

 Hata hivyo, vigogo wote waliosimamishwa kazi kwa agizo la JPM, wamepisha uchunguzi na wengine wako mahakamani ambapo itakapothibitika kuhusika katika ufisadi, kutanua huko kutageuka kuwa uchungu.

Leave A Reply