The House of Favourite Newspapers

Barakah Da Prince, meneja wake wazinguana

0

baraka prince (2)Stori: Musa Mateja

UONGOZI wa Kampuni ya Royal Nsyepa uliokuwa ukisimamia kazi za Mwanamuziki Baraka Andrew ‘Barakah Da Prince’, umeamua kusitisha usimamizi wa kazi za msanii huyo baada ya kuwepo kutokuelewana kati ya pande zote mbili.

Meneja wa msanii huyo, Mgalula Fundikira aliiambia safu hii kuwa, hivi karibuni Barakah aliwasilisha barua ya kusitisha mkataba akidai kuwa haoni mafanikio yoyote tangu awe na kampuni hiyo.

“Barakah amekuwa mtovu wa nidhamu, kafikia hatua ya kutuandikia barua akihitaji kuvunja mkataba wakati sisi ndiyo tumemfikisha hapo alipo. Tatizo ni tamaa na sisi tunaachana naye,” alisema meneja huyo.

Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Barakah ili azungumzie kilichotokea kati yake na uongozi wake lakini simu yake mara kadhaa ilikuwa ikiita bila kupokelewa. Jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

Leave A Reply