×

Denti wa darasa la sita ajinyonga

CHUGAStori: Stephano Mango, Risasi Jumamosi

RUVUMA: Simanzi! Mwanafunzi wa darasa la sita katika Shule ya Msingi Mashujaa iliyopo Mahenge katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Gloria Mrope (11) anadaiwa kujinyonga nje ya nyumba yao Mei 31, mwaka huu saa 12 jioni.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, ameliambia gazeti hili kuwa binti huyo alikutwa akiwa ananing’nia juu ya mti huku amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani.

Alisema marehemu alionwa na baba yake mzazi, Michael Mrope ambaye alikwenda kutoa taarifa kwa uongozi wa Serikali ya Mtaa na baadaye kituo kikuu cha polisi mjini Songea ambako askari walikwenda kuuchukua mwili huo kwa uchunguzi zaidi.

Uchunguzi wa awali, Kamanda Mwombeki alisema unaonesha hakukuwa na tatizo lolote la kifamilia ambalo lingeweza kuongoza mauaji hayo ambayo yamewaacha midomo wazi wakazi wa eneo la Mahenge alikokuwa akiishi marehemu huyo.

Leave a Comment