Mratibu wa semina ya wajasiriamali na mwakilishi wa Global Publishers Kanda ya Arusha, Chocks Francisco Chokala (mwenye suti) akiwa na baadhi ya wajasiriamali huko Arusha katika Hoteli ya New Safari.
…Akiendelea kusalimiana na wajasiriamali hao.
Mwalimu wa wajasiriamali, James Mwagamba (kushoto) akiwa na Francisco Chokala.
Wajasiriamali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya semina hiyo.
KAMPUNI inayochapisha magazeti pendwa Tanzania, Global Publishers, Jumamosi ilimwaga zawadi mbalimbali kwa washiriki wa semina ya wajasiriamali iliyofanyika Jumamosi iliyopita katika hoteli ya New Safari jijiniArusha. Mratibu wa Semina hiyo, Chocks Francisco Chokala, aliishukuru kampuni hiyo kwa kuijali jamii na kwa kuendesha bahati nasibu mbalimbali ikiwepo ambayo msomaji atajipatia nyumba kwa kujaza kuponi iliyo katika magazeti yote ya Global. Shindano hilo la nyumba linamalizika mwisho wa mwezi huu, ambapo msomaji mmoja atabahatika na kupata sifa ya kuitwa “baba au mama mwenye nyumba”!



