×

Tiko atumia Mwezi Mtukufu kupata mume!

Tikoooooooo

NA GLADNESS MALLYA

WAKATI waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa ndani ya swaumu, staa wa filamu Bongo, Tiko Hassan amefunguka kuwa na yeye yumo na ameamua kufunga kwa sababu mbili za msingi. Akipiga stori na Ijumaa, Tiko alisema licha ya kwamba kufunga ni nguzo muhimu ya Uislam lakini sambamba na hilo anakitumia kipindi hiki kumuomba Mungu amjalie apate mume na afanye vizuri kwenye fani yake.

“Namshukuru Mungu kwa kunifikisha kipindi hiki, niseme tu wazi kwamba safari hii nafunga nikinuia kabisa kuwa Mungu anijalie nipate mume maana nimechoka kuishi maisha ya kipweke.

“Pili, namuomba Mungu anijaalie katika fani yangu, kurwogana kumekuwa kwingi, watu hawapendani, Mungu aniepushe na shari,” alisema Tiko.

Leave a Comment