×

‘Ijumaa’ Toleo Jipya lakubalika Kwa Wasomaji

1.Waendesha bodaboda ambao ni wadau wa gazeti la Ijumaa toleo jipya wa eneo la Magomeni, wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa wa Global, Yohana Mkanda (wa kwanza kulia).

2.Wasomaji wa Ijumaa wa Magomeni wakipewa maelekezo na Mkanda (mwenye fulana nyeupe nyuma) namna ya kushiriki kujaza kuponi za bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

3Ijumaa, Jafari Hassan (kushoto) na Amani Jafari (katikati) ambao ni wasomaji wa Ijumaa, wakilisoma gazeti hilo. Anayewashuhudia kulia Mkanda aliyewakuta wakilisoma.

4.Msomaji Ijumaa aitwaye Rama Kajama (kushoto) akijaza kuponi ya kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

5.Mkanda (wa kwanza kushoto) akiwaelekeza wasomaji wa Ijumaa kurasa yenye kuponi ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

6 (2)Shuwea Midole (kushoto) na Farida Omari (kulia) wakipewa maelekezo kabla ya kujaza kuponi zao.

7.…Wakijaza kuponi.

8.Khatibu Hassan (kushoto) akijaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

9Alama Rashid (kushoto) na  Magongo Charles wakazi wa Mburahati jijini Dar wakisoma na gazeti la Ijumaa.

10.Magongo Charles (kulia) akisaidiwa na Mkanda kujaza kuponi yake iliyokuwa katika gazeti la Ijumaa.

11Mafundi gereji wa eneo la Mwenge Dar wakilisoma toleo jipya la Ijumaa huku wengine wakishika vipeperushi vya gazeti hilo.

12Msomaji wa Ijumaa akipewa maelekezo na Mkanda (kulia) namna ya kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

13

14..Mafundi gaereji wa eneo la Mwenge wakipozi na Mkanda huku wakisoma gazeti la Ijumaa.

 

IKIWA ni wiki ya pili tangu kuingia mtaani kwa tolea jipya la  gazeti la Ijumaa linalotoka kila siku ya Ijumaa likiwa na sura mpya na bei mpya ya shilingi 1,000, leo tena baadhi ya wasomaji jijini Dar walionekana kulikubali kwa kile walichoeleza kuwa lina mvuto wa aina yake na stori nzuri.

Maofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda na Jimmy Haroub, walitembelea maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam yakiwemo, Manzese, Magomeni, Mburahati, Mwenge na maeneo mengine  na kukuta wasomaji wa gazeti hilo wakilisoma na wengine wakinunua kwa muuzaji aliyekuwa karibu yao ambapo pia walishiriki kujaza kuponi za  bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

Akizungumza juu ya maboresho hayo, Mhariri wa gazeti hilo, Amran Kaima, alisema:

“Wasomaji wa habari za burudani nawaombeeni mzidi kulisoma gazeti la Ijumaa ambalo tumeliboresha zaidi kwa kuwa na habari nyingi za mastaa na kuwa na mwonekano mzuri, hivyo niwahakikishieni tutazidi kuliboresha na kupata maoni mbalimbali kutoka kwenu  ambayo tutayafanyia kazi.”

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Leave a Comment