×

Wanaoharibu Swaumu… wala Bakora

machangudoa (1)

Stori: Mwandishi Wetu, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Wakati Waislam wakiwa kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, kuna akina dada wanaoharibu swaumu za wanaume kwa kujiweka kingono ambapo hivi karibuni walijikuta wakichezea bakora za kutosha.

Tukio hilo lilinaswa na makamanda wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ Jumatano iliyopita katika mitaa ya Sinza Mori jijini Dar ambapo vijana kadhaa waliokuwa wakitoka msikitini, walionwa wakiwa wameshika bakora, huku wakionekana kutaka kufanya tukio f’lani.

machangudoa (2)OFM YAWAFUATILIA

Katika kujua kulikoni, OFM iliwafuatilia vijana hao waliokuwa wamevalia kanzu ambapo walipofika katika mitaa ya Meeda, walikutana na kundi la wasichana wanaojiuza wakiwa wamevaa kihasara na hapo ndipo walipoanza kuwacharaza bakora.

Kufuatia kashikashi hiyo, baadhi ya wasichana hao walifanikiwa kutoka nduki na kutokomea gizani lakini wawili waliokuwa ‘bwii’ walishindwa kukimbia ndipo walipokumbana na kibano hevi.

Wakati vijana hao wakifanya zoezi hilo, walisikika wakisema kuwa, wamewavumilia muda mrefu kwa tabia yao ya kujianika barabarani wakiwa nusu utupu lakini uzalendo umewashinda.

“Nyie hamjui kwamba huu ni Mwezi Mtukufu? Hamjui mnatuharibia swaumu zetu? Sasa leo mtakiona, kama Makonda (Paul, Mkuu wa Mkoa wa Dar) kawashindwa sisi tutawakomesha,” alisikika akisema mmoja wa vijana hao.

machangudoa (3)WAONEWA HURUMA

Baada ya kuchezea bakora za kutosha, wasichana walionaswa walionekana kuwa hoi na ndipo mmoja wa vijana hao alipowaonea huruma na kuwataka wenzake wawaachie kwa maelezo kuwa, kwa bakora walizochezea wakiendelea kufanya biashara ya kujiuza, watakuwa hawakomi.

MSAKO WAENDELEA

Baada ya kuwasambaratisha dada poa wa eneo la Sinza Mori, vijana hao walielekea maeneo ya Mapambano na Afrikasana kunakodaiwa kuwa na makahaba wengi. Hata hivyo, waliambulia patupu baada ya wasichana wa Mori waliokimbia kuwapa taarifa wenzao wa maeneo mengine kuwa kimenuka.

machangudoa (4)Wasikie vijana hao

Wakizungumza na OFM, vijana hao walioonekana kuwa na hasira, walisema wameamua kufanya oparesheni hiyo kwa kuwa wasichana hao wamekuwa wakiwaharibia swaumu zao ikiwa ni pamoja na kuwapa usumbufu wanapotoka au kwenda msikitini.

“Hawa wamekuwa wakitusumbua kila siku, siku za nyuma ukikatiza hapa (Mapambano) ukiwa unaenda msikitini au kwenye mambo yako mengine, wanakuzonga. Tumewavumilia vipindi vyote lakini kwa mwezi huu mtukufu imekuwa ni shida kubwa.

“Tumeanzisha zoezi hili na tutaendelea kila siku mpaka tuhakikishe wameondoka barabarani,” alisema kijana aliyejitambulisha kwa jina la Hamza Salum ambaye alidai ni ustaadhi wa madrasa moja iliyopo Mwenge jijini Dar.

SIYO MARA YA KWANZA

Tukio kama hilo la machangudoa kucharazwa bakora liliwahi kutokea kipindi cha nyuma maeneo ya Corner Bar (Sinza Afrikasana) baada ya ustaadhi mmoja kufanyiwa mchezo mchafu alipokuwa akienda msikitini kuswali swala ya alfajiri.

Katika tukio hilo, ustaadhi huyo alipokuwa anaenda kufanya ibada alikutana na madadapoa walioanza kujinadi kwake huku wakimchezeachezea, jambo lililomkasirisha sana.

Kufuatia kukerwa na vitendo hivyo, ustaadhi huyo alipofika msikitini aliwataarifu baadhi ya waumini wenzake ambao waliamua kuchukua bakora na kwenda kuwaadabisha.

NI KERO KUBWA

Wanawake wanaofanya biashara ya kujiuza maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar wamekuwa ni kero kubwa, si tu kwa waumini wa dini ya Kiislam bali hata waumini wa dini nyingine kutokana na tabia ya kuparamia kila mwanaume anayekatiza mbele yao.

Imeandikwa na Issa Mnally, Richard Bukos na Boniface Ngumije.

Leave a Comment