×

Msamy Afanyiwa Surprise Ya Gari Mazoezini

1Meneja wa msanii huyo, Rehema Jones (kushoto), akimkabidhi kadi ya gari Msamy muda mfupi baada ya kumfanyia Surprise hiyo.

2Msanii wa Filamu Bongo, Kajala Masanja (kushoto), akishuhudia surprise hiyo.

3Msamy akiwa ameshikiria faili la gari yake..

4…akizungumza na wanahabari.

5Kadi ya gari hiyo.

6Akishuka kwenye gari lake.

7Meneja wa Msamy, Rehema akimshukuru  Kajala kwa kumsaidia kufanikisha zoezi hilo.

8Msamy akiondoka na gari hilo.

9Gari lenyewe.

MSANII wa anayetikisa na ngoma yake ya Mabawa, Msamy Baby mapema leo uongozi wake umemfanyia Surprise ya gari aina ya Toyota Ipsum, akitokea mazoezini maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtandao huu meneja wa msanii huyo, Rehema Jones alisema kwamba, uongozi wao kwa ujumla umeamua kumzawadia gari hili kama moja ya zawadi yao ya siku yake ya kuzaliwa ambayo imepita wiki moja.

“Tumelazimika kumfanyia surprise hii kwakua siku ya birthday yake kama uongozi hatukushiriki kwa zawaidi yoyote na kwamba tulikuwa hatujakamilisha utaratibu wa usajili wa gari hili, hatukuwa na njia pekee ya kumuonyesha kama nasi tuko pamoja naye zaidi ya kufanya hivi,”

“Kweli Msamy hakujua kabisa kama kuna mpango huu na ndiyo maana utaona tumemfuata mazoezini kwake mapema hii na tukaamua kumshirikisha Kajala kama mtu wake wa karibu kwa kutaka asijue hata kidogo jambo hili hadi tutakapo mkabidhi, tumemchukulia gari kwakuwa ni mpenda magari, hivyo tunaamini roho yake itakuwa imesuzika kwani alilalamika sana siku ya birthday yake kuwa hatukushiriki ipaswavyo,” alisema Rehema.

Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.

 

Leave a Comment