×

Sabby Abadili namba, kisa mwezi mtukufu

sabby-2Stori: Imelda Mtema, Wikienda

DAR ES SALAAM: Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Sabrina Omary ‘Sabby’ amefunguka kuwa kufuatia usumbufu wa kwenye simu kutoka kwa wanaume wakware wanaoweza kutengua swaumu yake, ameamua kubadili namba kwa ajili ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza na Wikienda wikiendi iliyopita, Sabby alisema kuwa mwezi kama huu unahitaji kuepukana na vitu ambavyo vitakuingiza majaribuni kwa sababu simu ndiyo chanzo kikubwa hivyo ameona aipumzishe namba yake iliyozoeleka hadi mwezi huu wa toba uishe.

“Niliona nikiiacha wazi namba yangu iliyozoeleka nitatengua swaumu yangu kwa sababu ya wanaume wakware,” alisema Sabby aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Alikiba Saleh.

Leave a Comment