The House of Favourite Newspapers

Aina mbalimbali ya maumivu ya tumbo

0

Woman1Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo.

Maumivu chini ya mbavu kulia yanaweza kusababishwa na mawe kwenye mfuko wa nyongo, maambukizi kwenye mfuko wa nyongo Cholecystitis, uvimbe wa ini, jipu kwenye ini, saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo.

Maumivu chini ya chembe ya moyo husababishwa na vidonda vya tumbo, kiungulia, saratani ya tumbo na saratani ya kongosho.

Maumivu pembeni mwa kitovu husababishwa na mawe ya figo Kidney Stones, maambukizi ya figo, Pyelonephritis na  maambukizi kidoletumbo Acute Appendicitis

Maumivu chini ya kitovu huweza kusababishwa na maambukizi ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya zinaa kama klamidia, PID, vivimbe vya mji wa uzazi, mimba kuharibika na saratani ya kibofu cha mkojo.

Sababu nyingine za maumivu ya tumbo ni utumbo kujiziba Intestinal Obstruction,  utumbo kujisokota Volvulus, kula sumu na  mzio wa chakula fulani au ugonjwa wa Crohn Crohn’s Disease,  Ngiri Hernia au homa ya tumbo Typhoid Fever.

Kama unapata maumivu makali sana ya tumbo, yanajirudia au yanaambatana na dalili zozote kati ya zifuatazo basi onana na daktari mapema iwezekanavyo hasa kama una homa, kutapika matapishi yenye damu au kutapika sana, kukosa choo hasa ikiambatana na kutapika, tumbo kuvimba na kuumia.

Matibabu

Wakati ukielekea hospitali kwa ajili ya matibabu unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu kama Paracetamol au Diclofenac. Ukifika daktari atakufanyia vipimo kisha kukupa dawa.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz

Leave A Reply