Selebobo amkamata Shilole moja kwa moja
Oku Chigozie ‘Selebobo’
Stori: Boniphace Ngumije
MREMBO kutoka Bongo asiyekaukiwa matukio, Zuwena Mohammed ‘Shilole’ amefunguka kuwa msanii ambaye pia ni produza kutoka Nigeria, Oku Chigozie ‘Selebobo’ ameamua kumkamatia moja kwa moja kikazi ili kuhakikisha anasonga mbele na kuufikisha muziki wake kimataifa zaidi.
Zuwena Mohammed ‘Shilole’
Akichonga na gazeti hili Shilole akiwa katika maandalizi yake ya mwishomwisho ya safari kuelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki alisema mbele ya prodyuza huyo anategemea kuwa msanii mkubwa na akitoka Afrika Kusini ataelekea Nigeria kwa ajili ya maongezi zaidi na msanii huyo ikiwemo kufanya kichupa cha kolabo waliyofanya miezi michache iliyopita.
“Selebobo ameamua kufanya kazi na mimi moja kwa moja, nategemea atanifikisha mbali maana kama unakumbuka ndiye aliyemtoa Yemi Alade na wasanii wengi wenye majina makubwa Nigeria kwa sasa,” alisema Shilole.
KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP
*********
JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU:
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA
INSTAGRAM: @Globalpublishers
TWITTER: @GlobalHabari
FACEBOOK: @GlobalPublishers
SUBSCRIBE YOU TUBE: GlobalPublishers
GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE: @shigongotz