×

Diwani Chadema alivyohenyeshwa!

Amosi SipembaDiwani wa Kata ya Nyihongo, wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Amosi Sipemba (Chadema). Picha na Maktaba.

Na Shabani Njia, Ijumaa

SHINYANGA: Diwani wa Kata ya Nyihongo, wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga, Amosi Sipemba (Chadema) amejikuta akihenyeshwa na polisi baada ya kukamatwa kwa kudaiwa kuandaa kundi la vijana zaidi ya 20 ili walizuie jeshi la polisi kufanya kazi yake.

Tukio hilo lilitokea Juni 19, mwaka huu wakati wa maandalizi ya mkutano wa chama hicho kwenye Viwanja vya CDT wakati Chadema wakitaka kuzindua kampeni yao ya Oparesheni Okoa Demokrasia chini ya mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa chanzo, Sipemba akiwa miongoni mwa wahudhuriaji wa mkutano huo, alituhumiwa kuwaongoza vijana hao kukaidi amri ya polisi, hivyo kumpandisha kwa nguvu kwenye Difenda na kumfikisha kituoni sambamba na vijana hao kwa mahojiano. Akizunguza na gazeti hili baada ya kuachiwa kwa dhamana, Sipemba alidai kutofahamu lolote kuhusu vijana hao.

“Mimi sijaandaa vijana wowote kwa ajili ya kuzuia jeshi la polisi kufanya kazi yao ila nilichukuliwa kama mkumbo kwa sababu nilikuwa miongoni mwa vijana hao pasipo kujua dhamira yao, hata hivyo nashukuru Mungu nimetoka pamoja na wenzangu kwa dhamana ya shilingi laki tano kwa kila mmoja,” alisema Sipemba.

Leave a Comment