×

Isha; Mgonjwa wa chumba chake!

isha pichaIsha Mashauzi

MAMBO vipi mpenzi msomaji wangu wa Mpaka Home? Spidi yetu ni 120. Kwa kuonesha kuwa tunakujali wewe msomaji wetu leo tumewaletea mwanamuziki wa miondoko ya Taarab Bongo, Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ ambaye ni mmiliki wa Bendi ya Mashauzi Classic.

mashauzi (7)       Staa huyu anaishi Kinondoni Mkwajuni, katika nyumba ya kupanga ambayo wanaishi wawili tu; yaani yeye na mdada wake anayemsaidia kazi za nyumbani huku mtoto wake mwenye umri wa miaka 12 akiishi kwa bibi yake kijijini

Mpaka Home: Mambo vipi? Kwanza tupe ratiba yako ya siku nzima.

mashauzi (5)Isha Mashauzi: Mara nyingi ratiba yangu haikai vizuri kutokana na kazi zangu (maonesho ya usiku) lakini kama sikuwa na kazi usiku napenda sana kuamka mapema ili niweze kufanya usafi wa nyumba na kuandaa chakula kizuri ninachokipenda halafu nipate muda mzuri wa kupumzika kwa ajili ya kutengeneza sauti.

mashauzi (3)Mpaka Home: Nyumbani kwako kuna kila kitu kizuri ningependa kujua ni bidii yako mwenyewe au kuna shemeji anayekusaidia?

mashauzi (4)Isha Mashauzi: Hapana ni jitihada zangu mwenyewe maana siku hizi hakunaga hayo mambo, mwanamke bila kujishughulisha mwenyewe utabaki wa nyuma siku zote.

Mpaka Home: Kila mtu kuna sehemu muhimu nyumbani kwake anaipenda sana vipi wewe kwa upande wako ni sehemu gani unaipenda zaidi?

mashauzi (2)Isha Mashauzi: Ni chumbani kwangu, kwa kweli nakupenda sana.

Mpaka Home: Mastaa wengi wanapokuwa maarufu hawajichanganyi na majirani zao, vipi kwa upande wako?

Isha Mashauzi: Mimi sina tabia hiyo, mara nyingi natoka na kupiga nao stori moja mbili tatu maana hata nikipata shida wao ndiyo hunisaidia.

mashauzi (1)Mpaka Home: Una mpango wa kujenga?

Isha Mashauzi: Ndiyo, najenga maeneo ya Mbezi ya Kimara, nikikamilisha nitahamia hivi karibuni.

Mpaka Home: Nakushukuru sana kwa ushirikiano wako.

Isha Mashauzi: Ahsante sana na karibu tena!mashauzi (6)

Leave a Comment