×

Prezzo aeleza siri ya kolabo na Bamboo

prezzo (1)

Jackson Makini ‘CMB’ Prezzo.

RAPA mwenye jina kubwa Afrika Mashariki,  Jackson Makini ‘CMB’ Prezzo amefunguka kuwa siri ya kufanya kolabo na msanii mwenzake wa Kenya, Bamboo ni kutokana na kuendana kwao kikazi na kila wanapokutana siku zote hutengeneza ‘chemistry’ nzuri.

Prezzo

Akichonga na mtandao huu ‘direct’ kutoka Kenya, Prezzo ambaye amewahi kushirikishwa na Bamboo katika ngoma iitwayo Shika Nare aliongeza kuwa siku zote kila anapofikiria juu ya uwezo wa Bamboo hujikuta akitamani kufanya naye kazi.

“Bamboo ni msanii mzuri, ukicheki kwenye ngoma yetu hii mpya tuliyoshirikiana iitwayo Za Ovyo utaona kuwa Chemistry yake na yangu vinaendana sana,” alimaliza Prezzo.

Leave a Comment