×

Shinda Nyumba… Zimebaki Saa 192 Nyumba Hii Iwe Yako

1.         Na Richard Bukos

BAADA ya kuchukua miezi takriban sita tangu kuanza kwa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba inayoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers ambao ni watayarishaji wa Magazeti ya Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi na Championi, hatimaye zimesalia saa 192 nyumba hii ichukuliwe na unaweza kuwa ni wewe unayesoma makala haya.

8.Mkanda (kushoto) akimsaidia msomaji kukata kuponi baada ya kumaliza kuijaza.Jumatano iliyopita Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho aliwaongoza wanahabari wa vyombo mbalimbali kutembelea mjengo huo wa kisasa na kujionea jinsi ulivyokamilika.

Akiwa kwenye nyumba hiyo, Mrisho na kundi hilo la wanahabari waliikagua kila sehemu ambapo kila mmoja alijionea mjengo huo wenye samani za kisasa ndani yake.

8Miongoni mwa vivutio kwenye mjengo huo ni mandhari tulivu na upepo mwanana wa bahari unaovuma kwenye eneo hilo la Mbezi Salasala jijini Dar.

6Katika nyumba hiyo yenye kuvutia, imejengwa kwa vifaa madhubuti kuanzia marumaru, masinki, madirisha ya kisasa, mabomba na vifaa vinginevyo vyote vikiwa madhubuti na atakayeshinda atalazimika kubeba nguo zake tu kwani kila kitu kitakuwepo ndani.

10Mimi na wewe hatuwezi kujua nani atakayeibuka baba au mama mwenye nyumba, hivyo bado una nafasi ya kujishindia nyumba hiyo.

Ili uingie kwenye kinyang’anyiro cha kuweza kumiliki mjengo huu unachopaswa kwanza ni kununua Magazeti ya Global na kukata kuponi iliyopo katika magazeti hayo kisha kutuma sehemu husika.

13Ndugu msomaji, bahati hii haijirudii, kwa nini uendelee kuteseka kwenye nyumba za kupanga, kwa nini umtajirishe mwenye nyumba kila mwezi? Wakati ni huu! Jaribu bahati yako kwa saa 192 zilizosalia na kuitwa baba/mama mwenye nyumba jijini Dar kama hujawahi kuitwa hivyo.

11Hitimisho la bahati nasibu hiyo litakuwa Juni 30, mwaka huu kwenye Viwanja vya Zakhem vilivyopo Mbagala jijini Dar ambapo droo itachezeshwa chini ya uangalizi wa maafisa wa Bahati Nasibu ya Taifa na mwenye bahati yake kutangazwa mshindi.

Leave a Comment