Wiliam Samson (kulia) mkazi wa Vingunguti akijaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba. Anayemshuhudia ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.
Bakari Mkopole (kushoto) akipewa maelekezo na Mkanda kabla ya kujaza kuponi yake.
Japhary Mohamed (kulia) akijaza kuponi na Shabani Mhinda (katikati) akijadili jambo na Ofisa Masoko wa Global,Yohana Mkanda.
Wadau wa gazeti la Uwazi, Amani (kulia ) na Doto Daudi wakielekezana namna ya kujaza kuponi zao.
Ally Sosteny mkazi wa Vingunguti (kulia) akipewa maelekezo na Mkanda kabla ya kujaza kuponi.
KATIKA kuelekea kilele cha droo kubwa ya bahati nasibu ya ‘Shinda Nyumba’ iliyobakiza siku nane kuchezeshwa, leo Jumanne promosheni hiyo iliwafikia wakazi wa Vingunguti , Dar, waliojitokeza kwenye gari la matangazo kununua gazeti la Uwazi na kushiriki kujaza kuponi za bahati nasibu hiyo.
Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Maofisa masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda na Jimmy Haroub waliwafikia wasomaji katika mitaa mbalimbali ya maeneo ya Vingunguti huku wakizidi kuwahamasisha kushiriki.
Katika uhamasishaji huo, kama kawaida yake, Yohana Mkanda alirudia wito wake kwamba: “Siku zimebaki nane, hivyo nunueni magazeti ya Global mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka kuwa baba au mama mwenye nyumba! Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”
NA DENIS MTIMA/GPL