×

Watuhumiwa wa Mauaji ya Mwanza, Tanga Wauawa Dar

Kamanda Sirro

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema kuwa limefanikiwa kuwaua watuhumiwa wa mauaji yaliyotokea hivi karibuni katika mikoa ya Mwanza na Tanga.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya watu nane mkoani Tanga aliyefahamika kwa jina la Abuu Seif ameuawa juzi katika mapambano na askari maeneo ya Kimara jijini Dar, huku mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya Mwanza akiuawa maeneo ya Buguruni.

Leave a Comment