Nyumba ya Global aliyojishindia Nelly Mwangosi.
Hatimaye Nelly Mwangosi ameibuka mshindi wa nyumba ya Global Publishers Ltd jioni hii katika droo kubwa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mbagala Zakheem jijini Dar.
Nelly ni mama wa nyumbani mwenye umri wa miaka 45 anayeishi mkoani Iringa.
Akiongea baada ya kupigiwa simu na MC wa droo hii Mwangosi ameishukuru sana kampuni ya Global kwa kutoa zawadi hiyo ambayo itabadilisha maisha yake.