×

Satelaiti ya Juno yawasili Jupiter

juno-at-jupiter-exlarge-169 (2) Juno juno-at-jupiter-exlarge-169 (4) juno-at-jupiter-exlarge-169 (5) juno-at-jupiter-exlarge-169 (6) juno-at-jupiter-exlarge-169 jupiter-juno-auroras-exlarge-169

FILE - In this Friday, Aug. 5, 2011 file photo, an Atlas V rocket carrying the Juno spacecraft lifts off from Space Launch Complex-41 in Cape Canaveral, Fla. It was the first step in Juno's 1.7 billion-mile voyage to the gas giant planet, Jupiter. (AP Photo/Terry Renna)

juno (2) juno (3)

juonooSetilaiti ya Juno ya Shirika la Marekani NASA inayotumia nishati ya jua, imefika kwenye sayari ya Jupiter mapema alfajiri ya leo ikiwa ni miaka mitano tangu Agosti 5, 2011 ilipoanza safari ya kuelekea kwenye sayari hiyo.

Juno ilitua kwenye mhimili (orbit) ya Jupiter majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo kwa saa za Afrika Mashariki na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambapo inatarajiwa kudumu huko kwa muda wa mwaka mmoja na nusu ikifanya uchunguzi namna ambavyo sayari hiyo imeumbwa.

Kwa mujibu wa Kiongozi Mkuu wa Mpango huo kutoka NASA, Scott Bolton amesema hii ni historia mpya kwao na kwa ulimwengu wa Sayansi na teknolojia baada ya Juno iliyosafiri umbali wa kilometa bilioni 1.8 kutua huku ikikadiriwa kutumia mwendokasi wa 165,000 mph (265,000 kph) kuizunguka sayari hiyo pasipo msaada wa rubani wala kifaa chochote kutoka duniani.

Leave a Comment