MUUZA sura kwenye video za Kibongo, Ericka Daniel ‘Errycah’ amefunguka kuwa hakuna kitu anachokichukia duniani kama kuishi ndani ya ndoa kwa sababu yeye ni mtu anayependa maisha ya kuwa huru na siyo kuwa chini ya uangalizi wa mtu yeyote.
Akipiga stori safu hii, Errycah ambaye ameonekana kwenye video kadhaa za Kibongo ikiwemo ya Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’ iitwayo Kwa Hela, aliongeza kuwa katika dunia ya sasa suala la kuolewa si lalazima kama zamani badala yake mtu anaweza kuachana nalo kama anahisi halina mashiko kwake.
“Kiukweli ninachukia sana kuolewa, ninapenda kuwa mtu huru ambaye sibanwi na mtu yeyote yule, nafikiri kuwa single kwangu ni bora zaidi kuliko kuolewa,” alilonga Errycah.
