DAR ES SALAAM: Funguka! Mwigizaji aliyejipatia umaarufu kupitia Thamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jina Kabula’ amefunguka kuwa hana ugomvi na wanawake ambao walishawahi kuwa na uhusiano na mwanaume mmoja na yeye.
Akizungumza na Wikienda, Kabula alisema kuwa amejitengenezea tabia hiyo kwa kuwa hata anapogombana na mwanawake mwezake, kisa kikiwa ni mwanaume, haina faida kugombana naye, bora tu wakishajijua walipita sehemu moja ni kukaa pamoja na kuendelea na maisha kwa kuwa ilishatokea.
“Mimi kama unawajua ‘wake’ wenzangu wote, tunazungumza mpaka wengine ni marafiki wa damu. Mfano ni Jack wa Chuz (Jacqueline Pentzel),” alisema Kabula aliyezaa na Mwigizaji Tuesday Kihangala ‘Chuz’ aliyewahi kuwa mpenzi wa Jack wa Chuz’.
