×

Kaburi la Kanumba lavunjwa kichwani na miguuni!

KanumbaAliyekuwa nguli wa  lamu Bongo, Steven Kanumba

NA MAYASA MARIWATA RISASI MCHANGANYIKO

DAR ES SALAAM: KATIKA hali iliyohusishwa na imani za kishirikina, kaburi la aliyekuwa nguli wa  lamu Bongo, Steven Kanumba, lililopo makaburi ya Kinondoni limekukutwa likiwa limevunjwa pembe nne miguuni na kichwani na kuchotwa mchanga, Risasi Mchanganyiko lina ubuyu kamili.

kaburi la kanumba labomolewa (3)Tukio hilo la aina yake lilishuhudiwa na mtoa habari wetu mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo alimtonya paparazi wetu kuwa, kaburi la staa huyo limetobolewa na kuchotwa mchanga tofauti na yalivyo makaburi mengine ya eneo hilo.

kaburi la kanumba labomolewa (5)“Nilienda pale Kinondoni makaburini kutembelea kaburi la ndugu yangu ambalo lipo jirani tu na kaburi la staa huyo, cha ajabu nikaona hilo likiwa na matundu mawili upande wa kushoto (kichwani) na mawili kulia (miguuni) na isitoshe kwenye hivyo vitundu mchanga umechotwa, itakuwa ni mambo ya kishirikina, na ninahisi itakuwa wasanii wenzake wanataka nyota yake, si unajua tena,” kilisema chanzo hicho.

kaburi la kanumba labomolewa (6)PAPARAZI ATUA ENEO LA TUKIO

Baada ya kuunyaka ubuyu huo bila kupoteza muda paparazi wetu alifunga safari hadi eneo hilo na kushuhudia matundu hayo huku makaburi mengine yakiwa sawa.

kaburi la kanumba labomolewa (7)MASTAA WASHTUKA

Baada ya paparazi wetu kufotoa picha kadhaa, alizungumza na baadhi ya mastaa ambao waliomba hifadhi ya majina, kwa pamoja walionesha kushtushwa na taarifa hizo.

kaburi la kanumba labomolewa (1)“Hee! Ndiyo tunasikia kutoka kwako. Yaani kweli kaburi limebomolewa? Wamechimba mchanga? Mh! Makubwa kwa kweli sisi hatujui nini itakuwa kimesababisha hilo,” alisema mmoja wa wasanii wakubwa Bongo.

kaburi la kanumba labomolewa (8)MAMA KANUMBA ATIA NENO

Ili kutaka kufahamu ndugu wa marehemu wanazungumziaje suala hilo, Risasi Mchanganyiko lilimvutia waya, mama wa marehemu, Flora Mtegoa na kukiri kuifahamu ishu hiyo ambapo Jumapili iliyopita ali ka eneo hilo kwa lengo la kusa sha kaburi la mwanaye akashuhudia tukio hilo ambalo lilimfanya aangue kilio bila kupata majibu.

kaburi la kanumba labomolewa (4)“Siku ya kumbukumbu mwezi wa nne hapakuwa hivyo na baada ya hapo pia nilienda lilikuwa imara tu, cha ajabu nilivyoenda hiyo Jumapili nikapakuta hivyo ikabidi niokote vijiwe nizibe, huu ni ushirikina kabisa sipati jibu nani kafanya hivi nahisi mtu kavunja na nyundo ndo akachota mchanga, huenda wasanii wenziye wanataka kuchukua nyota yake kwa kuwa wanaona tangu afe bado jina linang’aa,” alisema mama Kanumba.

kaburi la kanumba labomolewa (9)RAIS TAFF ATOA NENO

Kama hiyo haitoshi, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Saimon Mwakifamba ili kusikia mtazamo wake kuhusu suala hilo ambaye naye aligusia suala la ushirikina.

kaburi la kanumba labomolewa (2)“Huo ni ushirikina tu ila siwezi kujua ni nani, kama ni wasanii wasirudie tena wafanye kazi kwa bidii tu, isitoshe wanaitia hasara familia kukarabati na huenda ni mtu wa kawaida katumwa afanye hivyo nyota yake ing’ae hatuwezi jua,” alisema Mwakifwamba.

Leave a Comment