×

Nay: Mamodo wa sauzi ni noma

Nay (11)Stori: MUSA MATEJA

Mwanamuziki Emmanuel Elbariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa anajisikia poa sana kufanya kazi na mamodo wa Sauzi kwani ni wajuzi wa kucheza na kamera na wanajua namna ya kumfanya msanii anayefanya nao kazi ajihisi ‘konfotabo’.

Akipiga stori na safu hii, Nay ambaye hivi karibuni alikwenda nchini humo kutengeneza kichupa chake cha Wimbo wa Saka Hela alisema kuwa, watu wamekuwa wakisifia muonekano wa video hiyo lakini warembo aliowatumia wamechangia kwa kiasi kikubwa.

“Kusema ukweli wale ma-video queen wa Sauzi ni noma, yaani naweza kusema ni profeshono maana ukiwa unashuti nao ni wepesi kukuzoea na kukufanya ujisikie kama umejuana nao siku nyingi, siwapondi wa Bongo lakini wa Sauzi ni zaidi,” alisema Nay.

 

Leave a Comment