BONIPHACE NGUMIJE
WADAU wa filamu mpo? Mzigo huu wa filamu hii unawahusu. Kuruthum Gita Langu ni moja kati ya filamu bora za Kibongo ambazo zimeshirikisha mastaa na watu wenye uwezo mzuri katika kuigiza.
Waigizaji wakuu katika filamu hii ni Banana Zorro, Irene Uwoya, Muhogo Mchungu, Asha Boko na wengineo.
Filamu hii imetungwa na Seveline Mtitu ambaye ni kaka wa aliyeiongoza, William Mtitu huku mwandishi wa script akiwa ni Richard Mziray na nyuma ya nyuma ya pazia (Behind the scene).
BONIPHACE NGUMIJE kamera alisimama Denis Ngakongwa.
Waandaaji wa filamu hii ambao 5 Effects wanasema imetumia muda wa wiki tatu lokesheni maeneo ya Bagamoyo na imegharimu zaidi ya milioni 20 za Kibongo. Bila ‘tantalila’ ingia lokesheni uone baadhi ya mtukio.
















