MBONGO Fleva anayetamba kwa Wimbo wa Jike Shupa, Naftari Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ amefunguka kuwa, miongoni mwa vitu ambavyo mpenzi wake havipendi ni kwenda kupiga kazi usiku kwani huwa anakuwa mpweke.
Akistorisha na safu hii, Nuh alisema suala hilo kwake limekuwa ni changamoto ya kila siku kwani ni vigumu kulikwepa, lakini hata anapokuwa anapata shoo za usiku, mpenzi wake huyo huwa hafurahii.
“Mpenzi wangu hupenda sana niwe naye usiku, nikiwa na kazi za studio au shoo muda huo hukubali nitoke kwa shingo upande,” alisema Nuh.
