×

Huyu ndiye mgombea mwenza wa Donald Trump

Davidson-MikePenceandtheTrumpVeepSweeps-1200

MGOMBEA wa Urais wa Marekani kwa tiketi ya Chama cha Republican, Donald Trump amemteua Gavana wa Jimbo la Indiana, Mike Pence kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi ujao utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.

Awali ilipangwa kuwa Trump amtangaze mgombea mwenza mapema tangu siku ya Ijumaa iliyopita lakini ghafla hiyo ilisitishwa kutokana na shambulio la kigaidi lililotokea jijini Nice, Ufaransa wiki iliyopita.

Aidha hapo awali ilitegemewa kuwa  Trump angewateuwa Spika wa Bunge la Marekani, Newt Gingrich au Gavana wa jimbo la New Jersey, Chris Christie kuwa mgombea mwenza kwenye uchaguzi huo ujao.

Mpaka sasa inakadiriwa kuwa Trump ameshatumia kiasi cha fedha zaidi ya dola milioni 55 kwenye kampeni za uchaguzi huo ambao atachuana na mpinzani wake kutoka kwenye chama cha Democratic, Bi. Hillary Clinton.

Hata hivyo Trump ameonekana kupingwa vikali na baadhi ya wanachama wa ndani ya chama chake kutokana na sera zake za ubaguzi.

Leave a Comment