×

Young D na madai ya Tunda kubwia unga

young-dee1KWENYE safu hii ya 10 Questions leo tunaye mwanamuziki wa kurap anayefanya vizuri kwenye Bongo Fleva, Young D ambaye amewahi kutamba na nyimbo kama vile Tunapeta, Ujanjaujanja, Hang Up, Siyo Mchoyo, Fununu na nyingine kibao. Amezungumza mengi na Mwandishi Wetu Gabriel Ng’osha kupitia maswali aliyoulizwa, fuatilia hapa chini…

Ijumaa: Vipi unaendeleaje kwa sasa baada ya kuachana na unga?

Young D: Maisha yanasonga kama kawa, niko vizuri sana nashukuru Mungu.

Ijumaa: Nini kinafuata baada ya kuacha dawa za kulevya?

Young D: Watanzania wategemee mambo mazuri, Young D mpya kwenye uongozi mpya na ulimwengu mpya kabisa.

Ijumaa: Hivi unga umetumia kwa muda gani vile?

Young D: Ni kweli nilitumia unga lakini siyo kivile na ndiyo maana haukunilostisha, sikutumia kwa muda mrefu.

Ijumaa: Ulikuwa unavuta katika mazingira gani?

Young: Mara mojamoja tena kwa kuwapa kampani washikaji, sijawahi kusema natumia mkwanja wangu mwingi kwenye kununua kilevi hicho.

Ijumaa: Vipi mpenzi wako Tunda, bado uko naye?

Young D: Tunda? Yupi huyo na niko naye kivipi?

Ijumaa: Yule modo aliyewahi kusema mlikuwa na mpango wa kuoana.

Young: Tunda hajawahi kuwa mpenzi wangu, alikuwa ni mshikaji wangu lakini hatukufikia hatua ya kuitana wapenzi.

Ijumaa: Lakini watu wenu wa karibu wanasema nyie ni wapenzi.

Young: Siyo kweli, hayo ni maneno ya watu tu.

Ijumaa: Na kwenye hili la kuvuta unga alishawahi kukupa kampani?

Young D: Kusema ukweli yeye hajawahi kuvuta hata siku moja.

Ijumaa: Wewe umeacha, unawashauri nini wale ambao bado wanaendelea na wale wanaotamani kutumia kilevi hicho?

Young D: Unga ni kitu kibaya sana, ukiingia huko ukakubuhu jua maisha yako yameharibika, ambaye hajawahi kutumia simshauri ajaribu na yule ambaye anavuta, namshauri afuate nyayo zangu.

Ijumaa: Kuna mtu yeyote unayeweza kumlaumu kwa kuingia kwenye matumizi ya unga?

Young D: Hakuna wa kumlaumu, ilikuwa ni akili yangu na akili yangu ndiyo iliyonituma niache.

Leave a Comment