Marehemu enzi za uhai wake.
Komediani ambaye pia alikuwa mgombea ubunge katika Jimbo la Masasi (CUF) kwenye uchaguzi Mkuu 2015, Ismail Issa Makombe maarufu kama Kundambanda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Marehemu Kundambanda ambaye enzi za uhai wake alikuwa anafanya kazi katika Kampuni ya Al-Riyam inayozalisha kipindi cha vichekesho cha Vituko Show kinachorushwa kwenye Runinga ya Channel Ten alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya ini kwa muda mrefu huku ikidaiwa kuwa wasanii wenzake wamemtelekeza.

Marehemu akiigiza enzi za uhai wake.
Marehemu alishiriki uchaguzi mkuu katika Jimbo la Masasi baada ya uchaguzi kwenye jimbo hilo kuahirishwa mwaka jana kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia chama cha NLD, Dkt. Emamanuel Makaidi.
Katika uchaguzi huo, Kundambanda aliambulia nafasi ya pili baada ya kupata kura 14,019 huku Bw. Rashid Chuachua wa CCM akipata kura 16,597 na kutangazwa mbunge wa jimbo hilo.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN
