KUNDI la Muziki wa Bongo Fleva, linaloundwa na wapendanao, Aika Mareale ‘Aika’ na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ limeitoa kimasomaso Bongo baada ya kutangazwa kama kundi pekee kutoka Bongo kushiriki kwenye Msimu wa Nne wa Coke Studio Afrika utakaoanza hivi karibuni kuruka kupitia vituo mbalimbali vya televisheni.
Katika msimu huu nchi sita zimeongezwa ambazo ni Ivory Coast, Cameroon, DRC Kongo, Ghana, Senegal na Ethiopia ambapo wasanii wapya walioingia kushirikiana kwenye kolabo ni pamoja na Kiss Daniel na Patoranking (Nigeria), Bahati (Kenya), Eddy Kenzo pamoja na Redio na Weasel kutoka Uganda. Wasanii wengine ni Kundi la Navy Kenzo (Bongo), Toofan (Togo) na Haile Roots kutoka Ethiopia.
