MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva ambaye anajivunia Wimbo wa Burgger Movie Selfie sokoni, Abedinego Damian amefunguka kuwa kila anapojikuta kwenye skendo zinazomhusisha na masuala ya mapenzi huwa anakuwa kwenye wakati mgumu kwa sababu watu wake wa karibu ambao ni wazazi na familia yake kwa jumla huwa hawapendi kabisa kumsikia katika skendo hizo.
Akichonga na gazeti hili, Belle alielezea wakati huo mgumu anaokutana nao ni pamoja na kuonekana kuwa hajatulia jambo ambalo wakati mwingine hufanya azinguane na mpenzi wake au kupata kazi kumuelewesha kuwa hakuna ukweli wowote katika skendo hizo bali watu wanajiongeza kutokana na kumuona akiwa na ukaribu na msichana anayehusishwa naye.
“Ukweli ni kwamba skendo za mapenzi huwa zinaniponza kwa watu ambao ninaheshimiana nao, sizipendi ndiyo maana huwa sipendi kabisa kuzipa nafasi kwa maana hazina faida yoyote kwangu,” alisema Belle 9.
Alipoulizwa juu ya skendo iliyowahi kumponza aligoma kufunguka na kudai hapendi kufufua mambo yaliyokwishapita.
