Na Gladness Mallya, RISASI MCHANGANYIKO
BAADA ya hivi karibuni ndoa yake kudaiwa kuvunjika, staa wa muziki na filamu Bongo, Flora Mvungi ameibuka na kusema wanaomuombea mabaya, wanambariki kwani yeye na mumewe wako imara.
Akipia stori na Za Motomoto News, Flora alisema watu wanamzushia mambo mengi kuhusu ndoa yake na Hamis Ramadhan ‘H. Baba’, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, hawatafanikiwa.
“Siwezi kuwazuia watu kuongea, nawaacha waongee maana wananibariki kwa maneno yao na ndoa yangu haivunjiki ng’o, tuko vizuri tunaendelea na maisha kama kawaida na mume wangu,” alisema Flora.