GAZETI namba moja kwa habari za kiuchunguzi na kijamii, Uwazi linalotoka kila Jumanne limegeuka na kuwa gumzo kila kona ya Jiji la Dar na vitongoji vyake kufuatia kuwepo pia kwa mikasa ya kusisimua, hadithi na simulizi zenye mashiko.
Wakazi wa Mambwepande na Mpigi Majohe, ambao Jumanne iliyopita walitembelewa na timu ya gazeti hilo ili kupata maoni yao, walisema Uwazi ni gazeti lililosheheni ambalo msomaji, anaona thamani ya hela aliyotoa kulinunua.
“Hili ni gazeti la watu, linagusa maisha yao kiasi kwamba unapotoa shilingi 500 yako wala hujutii. Mimi nalipenda, niwasihi wale ambao hawajawahi kulinunua, wafanye hivyo mara moja, hakika hawataacha kwa sababu lina sifa zote, linaelimisha, linaonya na kuburudisha,” alisema Rehema Shomari wa Mabwepande.
Kwa upande wa Afisa Masoko wa Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Amani, Risasi, Ijumaa Wikienda na Championi Yohana Mkanda alisema kuwa, wajibu wao ni kuhakikisha kila gazeti hilo linapotoka, linakuwa bora zaidi.