×

Wizkid asumbua na kiatu cha mil. 2

Wizkid-22-600x597MKALI wa muziki anayekimbiza kutoka Naija, Wizkid ameibukia mtaani akiwa amevalia kiatu aina ya Balenciaga A/W16 kilichotengenezwa na mbunifu maarufu duniani, Alexander Wang chenye thamani ya milioni mbili za Kibongo.

wizkid (2)Wizkid ambaye kwa sasa amejitanua zaidi kimataifa kupitia Ngoma ya One Dance aliyoshirikishwa na staa wa kimataifa, Drake ameonesha hajali gharama katika kununua viatu vya thamani.

wizkid (1) Viatu hivyo ameonekana kwa mara ya kwanza akiwa navyo mapumzikoni Houston, Marekani ambapo alisema; “Balenciaga ni moja kati ya viatu ninavyovipenda sana. Naweza kuvaa zaidi ya mara 100.”

Hii si mara ya kwanza kwa Wizkid kuvaa vitu vya thamani vya mbunifu huyo, kila kunapotokea matoleo mapya huwa kati ya watu wa kwanza kununua bila kujali gharama.

Leave a Comment