×

Bella kuipeleka nishike, Moshi

BELLAStori: BMM, Jumamosi

BAADA ya kuitambulisha kwa mara ya kwanza ngoma yake ya Nishike ndani ya Mango Garden, King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuipeleka ngoma hiyo pia kwa mara ya kwanza mkesha wa Sikukuu ya Nanenane ndani ya Ukumbi wa Hugos Garden, Moshi.

Akichonga na BMM, Bella anayebamba pia na ngoma kama Nashindwa, Nani Kama Mama, Nagharamia na nyingine kibao alisema kuwa video ya ngoma hiyo imetayarishwa Sauz ikiwa katika ubora wa hali ya juu kuanzia mazingira, madansa na hadi staili za kucheza.

“Nishike ni moja kati ya ngoma kali kuliko zote nilizowahi kuzitoa, kwa waliosikia watakuwa sawa na mimi, tukutane Jumapili hii mkesha wa Nanenane ndani ya Hugos Garden, Moshi kwa kiingilio cha Shilingi 10,000 tu,” alisema Bella.

 

Leave a Comment