×

Waziri Mkuu Majaliwa, Askofu Gwajima Wakutana Live

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo katika hafla ya harusi ya Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Amon Mpanju na mkewe Analises iliyofanyiak kwenye ukumbi wa jeshi wa Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akilishwa keki na mkewe, Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary walihudhuria katika tafrija hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju akimlisha keki mkewe , Analises katika tafrija ya harusi yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es salaam Agosti 6, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary Walihudhuria katika tafrija hiyo.
IKIWA ni takribani mwezi mzima sasa tangu Askofu wa Kanisa la Uzima na Ufufuo la Jijini Dar es Salaam, Josephat Gwajima kutoa shutuma akihubiri kanisani kwake kwa baadhi ya viongozi na wanachama wa CCM kuwa wanafanya mipango ili rais John Pombe Magufuli asikabidhiwe Uenyekiti wa Chama hicho, jambo ambalo lilipelekea Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar kumtafuta ili ajibu tuhuma za kile walichokiita kuwa ni kauli za kichochezi.
Juzi Jumamosi, Agosti 6, Askofu Josephat Gwajima alikutana uso kwa uso na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungno wa Tanzania, Kassim Majaliwa na kusalimiana tena kwa kuchangamkiana, jambo ambalo liliwashangaza baadhi ya watu waliokuwepo kwani hawakutegemea kama hali kama ile ingetokea huku ikilinganishwa kauli tata za Gwajima ambazo amekuwa akizitoa kanisani kwake kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa CCM na serikali.
Tukio hilo lilitokea Juzi Jumamosi, Agosti 6 wakati walipohudhuria sherehe ya harusi ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba, Amon Mpanju na mkewe, Analises iliyofanyika kwenye ukumbi wa Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.
TUJIKUMBUSHE
Baada ya Askofu Gwajima kumshutumu kwa rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa hataki kumpa Uenyekiti wa chama hicho, rais Magufuli, Askofu huyo alitoweka nchini na kuelekea Japani ambako alikaa siku kadhaa na kupelekea jeshi la polisi kumtafuta bila mafanikio, baadaye alirejea nchini, siku aliposhuka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarrage Nyerere jijini Dar alikamatwa na Jeshi hiulo na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwenda kujibu tuhuma zilizokuwa zikimkabiri.

Profesor Jay “Mazuri na Mabaya ya Serikali ya Magufuli Niliyoyaona ni Haya Hapa’

Leave a Comment