×

Mama amsaka mrithi wa Kanumba

KanumbaMarehemu Steven Kanumba

Stori: Mwandishi Wetu, Wikienda

DAR ES SALAAM: Mama mzazi wa aliyekuwa kinara wa sinema za Kibongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ameanza harakati za kumsaka mrithi wa mwanaye huyo kwa kuanzisha shindano alilolipa Jina la Kanumba Star Search (KSS) ya AM Arts Promotions chini ya Mwanaidi Hassan Matanga na KZG Mobile Phone.

mamakanumbaaa.jpgMama Kanumba

Akizungumza na Wikienda, Mama huyo alisema kuwa shindano hilo litaanza Septemba 2, mwaka huu, likianzia mikoani ambapo litamalizikia jijini Dar, lengo akishirikiana na Kampuni likiwa ni kupatikana kwa mtu atakayeendeleza kipaji cha staa huyo aliyefariki dunia Aprili 7, 2012.

“Tumejipanga kufanya shindano hili na iwapo Mungu akipenda, tutaanza mwezi ujao mikoani na fainali itafanyika hapa (Dar),” alisema Mama Kanumba.

Profesor Jay “Mazuri na Mabaya ya Serikali ya Magufuli Niliyoyaona ni Haya Hapa’

Leave a Comment