_kim-kardashian-kanye-west-MWANAMITINDO maarufu duniani Kim Kardashians, ameingiwa hofu na kuomba msaada wa kisaikolojia kuhusu kuambukizwa virusi vya ugonjwa hatai wa Zika unaosambaa hasa katika Bara la Ameika.

Tukio hilo limetokea wikiendi iliyopita wakati mwanadada huyo ambaye ni mke wa rapa  Kanye West wakati akifanya kipindi chake cha televisheni cha Keeping Up With the Kardashians huku akionekana kuwa na hofu kubwa moyoni mwake  kuhusu kuambukizwa viusi hivyo.

“Ninashangaa, itakuwaje kama tukifanyiwa vipimo na nikagundulika nimeambukizwa Zika kabla hatujaudi nyumbani?” Kim alisema. “Ninawaondoa hofu.”

“Ulishawahi kung’atwa na mbu?” Kourtney alimuuliza Kim.

“Hapana, wewe je?” Kim alijibu.

“Hapana,” Kourtney alimuuliza Kim.

Kim na Kourtney ambao wapo nchini Cuba na watoto wao pamoja na mumewe,  Kanye West, Khloe Kardashian and Malika Haqq na msaidizi wao Stephanie wote walionekana kuwa na wasiwasi kuhusu afya ya kila mmoja wao endapo watapimwa huko ugenini!