×

Amani Latinga Msasani, Wasomaji Walichangamkia

2Wasomaji wa Gazeti la Amani wakiongozwa na Haji Juma (katikati) wakilisoma gazeti hilo.

GAZETI la Amani leo lilitinga maeneo ya Msasani na sehemu nyingine za jiji la Dar es Salaam ambapo wasomaji walilichangamkia kulinunua.

9Jimmy Haroub akimsaidia msomaji wa Amani kulifungua gazeti hilo.

Akizungumza na wakazi eneo la Msasani, jirani na kituo cha daladala kiitwacho Macho (CCBRT), Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers inayozalisha gazeti hilo pamoja na Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, Yohana Mkanda, alisema anawaomba wasomaji wa magazeti hayo ya Global kuendelea kulinunua Amani kwa bei ya Sh.500 kwani limesheheni habari nyingi za burudani, hadithi, machombezo na mikasa.

8Mwanadada huyu akilisoma Gazeti la Amani eneo la Kituo cha Daladala cha Msasani.

“Magazeti yote ya Global yanauzwa kwa shilingi 500 isipokuwa Ijumaa pekee lenye muonekano mpya ndilo linauzwa shilingi 1000. Nawasihi wasomaji wetu waendelee kununua magazeti yetu ili wazidi kuhabarika, kuelimika na kuburudika,” alisema Mkanda.

3.Mbwana Rashid akisoma Gazeti la Amani eneo la Kituo cha Daladala cha Macho, Msasani.

5..Mdau wa Gazeti la Amani akifafanuliwa jambo na Jimmy Haroub (kushoto).

7Mmasai aitwaye Aloyce Malongo akilisoma Gazeti la Amani.

1Msomaji wa Amani aitwaye Kara Jayler Mkazi wa Msasani akisoma gazeti hilo.

4.Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub (kulia) akiwashuhudia wasomaji wa Amani wakilisoma gazeti hilo.

6Ofisa Usambazaji wa Global, Jimmy Haroub (kushoto) akimfuatilia msomaji wa Amani.

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment