×

Shigongo Aongoza Waombolezaji Kuaga Mwili wa Mama wa Mhasibu wa Global

MSIBA MAMA SHAMIM (1)Jeneza lenye mwili wa marehemu, Bi. Halima Mohamed Mshana ambaye ni mama mzazi wa mhasibu wa Kampuni ya Global Publishers, Shamim Mshana likiingizwa kwenye gari katika Hospitali ya Lugalo, Dar tayari kwa safari ya kuelekea Moshi, Kilimanjaro kwa mazishi.MSIBA MAMA SHAMIM (2) MSIBA MAMA SHAMIM (3) MSIBA MAMA SHAMIM (4) MSIBA MAMA SHAMIM (5) MSIBA MAMA SHAMIM (6)Jeneza lenye mwili wa marehemu, Bi. Halima Mohamed Mshana ambaye ni mama mzazi wa mhasibu wa Kampuni ya Global Publishers, Shamim Mshana likiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Moshi, Kilimanjaro kwa mazishi. MSIBA MAMA SHAMIM (7)Mhariri wa Gazeti la Uwazi (mbele kushoto), Elvan Stambuli pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Global Publishers wakiwa katika huzuni wakati wa kuaga mwili wa marehemu. Nyuma kushoto ni Mkurugenzi Eric Shigongo pamoja na Mhasibu Lawrence Kabende (mwenye shati la bluu).MSIBA MAMA SHAMIM (8)Mtoto wa marehemu, Shamim Mshana (kushoto) akipewa pole na waombolezaji. MSIBA MAMA SHAMIM (9) MSIBA MAMA SHAMIM (10)

Shamim akipanda kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Moshi kwa mazishi.

Dar es Salaam

LEO Agosti 12, 2016, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo amewongoza waombolezaji kuuaga mwili wa marehemu Bi. Halima Mohamed Mshana ambaye ni mama mzazi wa Mhasibu wa Kampuni ya Global Publishers, Shamim Mshana katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

Bi. Halima Mohamed Mshana alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya TMJ ya jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. Mwili wa marehemu ulitolewa jana hiyo na kupelekwa katika Hospitali ya Lugalo kuhifadhiwa ambapo leo shughuli ya kuaga imefanyika na kuusafirisha kuelekea Moshi kwa ajili ya mazishi.

PICHA NA DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment