Almaz Ayana ameshinda medali ya dhahabu ya kwanza Rio na kuvunja rekodi ya dunia.
Rio, Brazil
Mwnariadha Raia wa Ethiopia, Almaz Ayana amekuwa Mwafrika wa kwanza kushinda medali ya dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki mjini Rio 2016 na kuvunja rekodi ya dunia mbio za mita 10000 (sawa na kilomita 10) za wanawake.
Ayana aliwaacha nyuma wapinzani wake mbio zikiwa katikati na kuendelea hadi mwisho akimaliza mbio za kilomita 10 kwa kutumia muda wa dakika 29 na sekunde 17.45.
Rekodi ya awali iliwa 29:31.78 na iliwekwa na Mchina Wang Junxia mwaka 1993 kwenye michuano hiyo. Mkenya Vivian Cheruiyot ameshinda fedha naye raia mwingine wa Ethiopia Tirunesh Dibaba akachukua shaba.