Eric Shigongo akitoa semina ya Mambo 10 ya Kufanya ili Kufanikiwa Wakati wa Hali Ngumu ya Uchumi kwa wakuu wa wilaya wastaafu.


Wakuu wa wilaya wastaafu wakiwa makini wakati wa semina ya Shigongo.
Shigongo akisisitiza jambo kwa wakuu wa wilaya wastaafu wakati wa semina hiyo iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Aliyekuwa Mkuu Wilaya ya Wanging’ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela akifurahia somo la Shigongo.
Mmoja wa wakuu wa wilaya wastaafu akinyoosha mkono kumuuliza swali Eric Shigongo.

Shigongo akijibu maswali ya wakuu wa wilaya wastaafu.
Semina ikiendelea.
Shigongo akisalimiana na wakuu wa wilaya wastaafu baada ya semina hiyo.
MWANDISHI na mhamasishaji mahiri Afrika ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo James, leo ametoa semina ya ujasiriamali kwa wakuu wa wilaya wastaafu.
Semina hiyo iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF imefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye jengo la PSPF jijini Dar es Salaam.
Katika semina iyo, Shigongo amefundisha Mambo 10 ya Kufanya ili Kufanikiwa Wakati wa Hali Ngumu ya Uchumi.
Mambo hayo aliyoyafundisha mjasiriamali huyo ni pamoja na;
- Usibabaike
- Chambua na chukua hatua
- Badili mkakati
- Usipoteze mwelekeo
- Hakikisha unakuwa bora, wape watu suluhisho
- Endelea kuwa na sifa, mwenendo mwema
- Anzisha vyanzo vingi vya mapato
- Anza kununua, si kuuza
- Chakarika zaidi
- Endeleza uhusiano wako na Mungu
Shigongo alisema kuwa mambo hayo 10 ndiyo ambayo mtu akiyafanya wakati wa uchumi mbaya, hakika atatengeneza fedha nyingi na kufanikiwa zaidi wakati wengine wote wanafunga biashara, yeye atakuwa anafungua biashara nyingine mpya.
Habari: Clarence Mulisa; Picha: Hilaly Daud / GPL








